Alhamisi, 7 Agosti 2014

TAZAMA KIJANA AKITONGOZWA NA MALAYA.



Methali 7
1 Mwanangu, yashike maneno yangu,Na kuziweka #amri zangu akiba
kwako.

2 Uzishike amri zangu ukaishi,Na sheria yangu kama mboni ya jicho lako.

3 Zifunge katika vidole vyako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu;Mwite ufahamu jamaa yako mwanamke.

5 Wapate kukulinda na #MALAYA,Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.

6 Maana katika dirisha la nyumba yanguNalichungulia katika shubaka yake;

7 Nikaona katikati ya #WAJINGA
,Nikamtambua miongoni mwa vijana, #KIJANA mmoja asiyekuwa na akili,

8 Akipita njiani karibu na pembe yake,Akiishika njia iendayo nyumbani kwake,

9 Wakati wa magharibi, wakati wa jioni,Usiku wa manane, gizani.

10 Na tazama, mwanamke akamkuta,Ana mavazi ya #KIKAHABA
mwerevu wa moyo;

11 Ana kelele, na ukaidi;Miguu yake haikai nyumbani mwake.

12 Mara yu katika njia kuu, mara viwanjani,Naye huotea kwenye pembe za kila njia.

13 Basi akamshika, akambusu,Akamwambia kwa uso usio na haya,

14 Kwangu ziko sadaka za amani;Leo hivi nimeziondoa nadhiri zangu;

15 Ndiyo maana nikatoka nikulaki,Nikutafute uso wako kwa bidii, nami nimekuona.

16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri,Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
,
17 Nimetia kitanda changu manukato,Manemane na udi na mdalasini.

18 Haya, na tushibe upendo hata asubuhi, #Tujifurahishe nafsi zetu kwa
#mahaba.

19 Maana #mume wangu hayumo
nyumbani,Amekwenda safari ya mbali;

20 Amechukua mfuko wa fedha mkononi;Atarudi wakati wa mwezi mpevu.

21 Kwa maneno yake mengi na ulaini #akamshawishi,Kwa ubembelezi wa
midomo yake akamshinda.

22 Huyo akafuatana naye mara hiyo,Kama vile ng’ombe aendavyo #MACHINJONI;Au mpumbavu
kuadhibiwa katika pingu;

23 Hata mshale umchome maini;Kama ndege aendaye haraka mtegoni;Wala hajui ya kuwa ni hasara ya nafsi yake.
*****************************************
HIZO NI HEKMA ZA MFALME SELEMANI, JAMANI TUAMKE.

PISHI CHINI YA ARDHI


***CAMP CRAFT ***

Hii ni moja ya ufundi kambini ktk kipengele cha
MIOTO na MAPISHI.

AINA hii ya pishi linalotumia MOTO usio na mafiga wala jiko, HUTUMIKA sana ktk kambi LA mfunzo ya Vijana.

Mtu yeyote aliyeko porini
Njia hii inamfaa sana. Pale akosapo Vifaa vya kupikia mjumban alivyovizoe.
**Kama Sifuria ,Chungu , nk.

Pishi lifaalo ktk UPISHI huu ni #UGALI Mkate ,nk.

Hebu Leo tuangalie
.pishi la #UGALI"

VIAMBA UPISHI :
.>Maji safi.
.>Unga wa ugali.

****.#VIFAA**
1: Majani ya mgomba au majani yoyote mapana yasiyo na sumu.
2: Mfuko wa plastic.
3: Mwiko au kijiti imara toka kwenye mti usiyo na sumu.
4:Chanzo cha moto wa kuni au mkaa.

>>Chimba shimo la umbo lolote upendalo, kulingana na UMBO LA MCHANGANYIKO wa ugali wako (kama tutakavyoona hapo chini)
Ila kina chake kiwe NCHI 4. ,
Jitahidi kuchimba sehemu isiyo na unyevu.
......Upana wa shimo uzidi mzunguko wa ugali kwa NCHI 2.

HATUA ZA KUANDAA PISHI HILI ZURI LA KUVUTIA :

>>Changanya unga wako na maji baridi mpaka uwe katika hali ya dongo zito…

>>Utengeneze uwe umbo bapa, unene wa NCHI 1. Mpaka NCHI 1.5.
L
>>Uweke mchanganyiko wako, kwenye majani tajwa hapo juu (yalooshwa vyema) yapata gamba 1. ,

>>Kisha gamba 1. La mfuko wa plast lifuate juu ya gamba la majani,,

>>kisha gamba moja tena la majani lifuate juu ya gamba la plastiki.

>>Alafuuu Weka mchanganganyiko wako ndani ya shimo lenye size yake,

>>Sambaza udongo juu yake yapata NCHI 1.mpaka 1.3.

>>Washa moto juu ya mchanganyiko wako, Kisha chochea kuni za kutosha/moto wa uhakika , kulifunika shimo ZIMA, kwa muda wa dakika 10. - 15.
Usiuache moto kufifia.

>>FUKUA UGALI WAKO uondoe kwenye MAGAMBA Utakuwa tayari kwa kuliwa.
NISALAMA kwa afya yako.
..............Tamati......
Next time Tutajifunza jinsi ya KUPIKA juu ya #MAJI. ni Rahisi sana.Mungu atupe uzima tu. Kwa Neema.
*****************************

@Prepared by.
Joel P.Majumbi.
(Maskin Waroho)

Kwa maelezo zaidi:
Tel..0754-950-444
0715-950-444
0782-950-444
>E.mail
.majumbijoel@gmail.com.